Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JS Saoura waichimba Simba, CAF yataja waamuzi

34809 Pic+simba Tanzania Web Photo

Fri, 4 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Klabu ya JS Saoura, anayoichezea, Thomas Ulimwengu, imeanza kuifuatilia Simba kila hatua baada ya kupangwa kundi moja la D katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.

Simba na JS Saoura zitacheza Januari 12 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kuonyesha kuwa wanaifuatilia Simba kwa karibu, mtandao wa klabu hiyo, wameposti kipande cha video kikionyesha umati wa mashabiki wa Simba uliojitokeza kwenye mchezo wao wa marundiano ya raundi ya kwanza dhidi ya Nkana Red Devils.

Waalgeria hao, wameonekana kushangazwa na idadi kubwa ya mashabiki waliojitokeza Uwanja wa Taifa kuisapoti Simba ambayo ilipindua matokeo ya mabao 2-1, waliyofungwa Kitwe, Zambia kwa kushinda mabao 3-1.

Ukiachilia mbali wingi huo wa mshabiki pia JS Saoura iliufuatilia mchezo uliopita wa Simba dhidi ya Singida wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Kupitia mtandao wao wameandika tena kuwa wapinzani wao Simba wameshinda mchezo wa ligi dhidi ya Singida United huku nyavu zao zikiwa hazijaruhusu bao kwenye mchezo huo.

Anayetajwa zaidi katika mtandao huo kama mtu hatari kwenye kikosi cha Simba ni kiungo Clatous Chama kutokana na uwezo wake wa idadi ya mabao aliyoyafunga kwenye michuano hiyo mikubwa zaidi Afrika ngazi ya klabu.

Chama ana mbao manne kwenye orodha ya wafungaji kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, aliyafunga mabao hayo kwenye mchezo wa awali dhidi ya Mbabane Swallows, ulioanza kucheza jijini Dar es Salaam, Novemba 28.

Katika mchezo huo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 na kwenye idadi hiyo Chama alifunga bao moja kwenye mchezo wa marudiano, Desemba 4 mwaka jana kiungo huyo alipachika mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 4-0.

Bao la nne la Chama liliibeba Simba kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Nkana Red Devils, kiungo huyo alipiga bao la tatu ambalo liliihakikishia Simba nafasi ya makundi.

Wakati kule akitajwa Chama, nyumbani Tanzania anayetajwa zaidi kwenye kikosi cha JS Saoura ni Thomas Ulimwengu ambaye ametua kwenye timu hiyo kuwaongezea nguvu.



Chanzo: mwananchi.co.tz