Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKU yazidi kubomoka

Simba Vs JKU LEO JKU yazidi kubomoka

Thu, 4 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha JKU kinazidi kupukutika baada ya timu za bara kuendelea kung’oa wachezaji kutoka kwenye timu hiyo sasa ni zamu ya kipa Yacoub Suleiman Ali ambaye amesainiwa na JKT Tanzania.

Hadi sasa JKU imetoa mastaa wake wanne ambao ni viungo wawili mmoja akisajiliwa na Yanga Shekhan Ibrahim, Saleh Masoud Karabaka (Simba), Gamba Idd Matiko na Yakub aliyemalizana na JKT.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya uongozi huo kimeliambia Mwanaspoti kuwa dili la kipa huyo ambaye kwasasa hatumiki kikosini limeshamalilika na muda wowote atatambulishwa na timu yake mpya.

“Ni kweli ni idadi kubwa ya wachezaji wametoka hilo kama viongozi tumekaa na kulizungumza licha ya kuingiza fedha tunahofia kushindwa kutwaa taji msimu huu kutokana na kuondoa mastaa wengi;

Penetration Testing Services Might Be Cheaper Than You Think ! Penetration Testing Services | Search Ads by TaboolaSponsored Links “Malengo yetu ni kutwaa taji la msimu huu lakini ondoka ondoka ya wachezaji inatutisha kwasababu mbali na sajili hizo nne bado kuna ofa nyingine mezani,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa kocha wa timu hiyo, Salum Ali Haji kwaajili ya kuzungumzia ondoka ondoka ya wachezaji wake alisema amezungumza na uongozi kuhusiana na hilo wamemuahidi kuongeza nguvu kwa kusajjili wachezaji wengine.

“Utafanyika usajili wa wachezaji wengine kwaajili ya kuzipa mapengo na wengine watapandishwa kutoka timu ya vijana hivyo naamini kila kitu kitaenda sawa.” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live