Wawakilishi wa Zanzibar kwenye michuano ya CAF, KMKM na JKU zimeamua kuhamishia mechi zao za kimataifa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi kutokana na viwanja viwili vya kisiwani humo kuwa kwenye ukarabati mkubwa.
KMKM inajiandaa kucheza mechi za raundi ya awali dhidi ya St George ya Ethiopia ikiwa ni mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati JKU itacheza Kombe la Shirikisho Afrika na Singi-da Fountain Gate ya Tanzania Bara, mechi zikipigwa kati ya Agosti 18-20.
Viwanja vya Amaan uliopo Unguja na ule wa Gombani (Pemba) vipo kwenye marekebisho makubwa ya kisasa na inaelezwa marekebisho hayo huenda yakamalizika kati ya Novemba hadi Disemba mwaka huu, hivyo sio rahisi kwao kuvitumia viwanja hivyo.