Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKT: Ubingwa na suala la muda tu

JKT Queens JKT: Ubingwa na suala la muda tu

Wed, 29 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Nahodha wa JKT Tanzania, Donisia Minja amesema siri ya kikosi chao kuwa bora msimu huu ni kuzingatia mazoezi na kutiana moyo huku akitamba kuwa ubingwa ni suala la muda tu. JKT Queens iko nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 28 pointi moja nyuma ya Fountain Gate Princess iliyo kileleni kwa pointi 29.

Donisia mwenye mabao tisa akiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ufungaji bora alisema msimu huu wamepania kuhakikisha wanarejesha heshima ya timu hiyo.

Alisema kama nahodha anafurahi kuona kila mchezaji katika kikosi hicho anapambana kuhakikisha malengo yao ya ubingwa msimu huu yanatimia.

"Tuko fiti kwa sababu tunazingatia mazoezi na kutiana moyo uwanjani na kama unavyojua hii ni timu ya jeshi lazima tuwe ngangari.

"Huwa tunafanya mazoezi mara moja tu asubuhi lakini kuna wakati baadhi tunajiongeza kufanya mazoezi ya ziada ndio maana wengi wanatuona hatuchoki haraka kwenye mechi zetu, "alisema Donisia

Donisia alisema anajua kuwa mbio za ubingwa kwa timu nne za juu ni kubwa lakini watahakikisha wanacheza mechi zao sita zilizobaki kwa mahesabu ili kuhakikisha malengo yao ya ubingwa yanatimia.

"Ligi ngumu sana na vita ya ubingwa kwa timu nn, Yanga, Simba, JKT ni Fountain Gate ni kubwa sana sasa kwa mechi zilizobaki hatutakiwi kuteleza ni kucheza kwa mahesabu tu ili jambo letu litimie," alisema Donisia ambaye msimu huu yuko katika kiwango bora.

Chanzo: Mwanaspoti