Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKT Tz, KMC zaenda suluhu

IMG 8996.jpeg JKT Tz, KMC zaenda suluhu

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, JKT Tanzania wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Jana Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.

Kiungo Najim Magulu alianza kuifungia JKT Tanzania dakika ya nane, kabla ya mshambuliaji Shaaban Iddi Chilunda kuisawazishia KMC dakika ya 40.

Kwa matokeo hayo, JKT Tanzania inafikisha pointi 18, ingawa inabaki nafasi ya 12, wakati KMC imetimiza pointi 24 katika mchezo wa 18 nayo inabaki nafasi ya tano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live