Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKT Tz, Ihefu hakuna mbabe Chamazi

IMG 6343.jpeg Kiungo wa JKT Tz Said Ndemla

Sun, 26 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya JKT Tanzania imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Kiungo Said Hamisi Ndemla alianza kuifungia JKT Tanzania dakika ya 14, kabla ya mshambuliaji Ismail Mgunda kuisawazishia Ihefu SC dakika mbili baadaye.

Kwa sare hiyo, JKT Tanzania inafikisha pointi 15 na kusogea nafasi ya saba, wakati Ihefu SC imetimiza pointi tisa katika nafasi ya 13 baada ya wote kucheza mechi 11.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live