Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKT Tanzania yamnasa Hassan Nassor

JKT Tanzania Kikosi cha JKT Tanzania

Fri, 30 Jun 2023 Chanzo: Dar24

Kiungo kutoka Visiwani Zanzibar Hassan Nassor ‘Machezo’ amezikacha Simba SC Simba SC na Singida Big Stars, kufuatia kuwa katika hatua za mwisho kumwaga wino JKT Tanzania iliyopanda Ligi Kuu Bara kutoka Ligi ya Championship.

Machezo alikuwa akiichezea Mbeya City iliyoshuka daraja baada ya kuzidiwa ujanja na Mashujaa FC ya Kigoma, kwa sasa yupo huru baada ya kumaliza mkataba na timu hiyo ya jijini Mbeya iliyomaliza msimu wa Ligi Kuu Bara ikishika nafasi ya 14 na kucheza ‘Play-Off’ na KMC FC na kupigwa kwa jumla ya mabao 3-2 kisha kuangukia mikononi mwa Mashujaa iliyowanyoa kwa mabao 4-1 na kuishusha.

Inaelezwa kiungo ameshamalizana kila kitu na JKT Tanzania iliyorejea katika ligi hiyo baada ya kushuka misimu miwili iliyopita.

Hata hivyo, Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Malale Hamsini amesema kuwa, timu hiyo inaendelea na maboresho ya msimu ujao ila kuhusu usajili watatangaza dirisha likifunguliwa.

“Wachezaji tunaowalenga ni wale wazoefu ambao tunaamini watatusaidia, wapo ambao tutaachana nao kama ilivyo utaratibu kila msimu unapoanza lakini wengine tutaboresha tu mikataba yao,” amesema Malale aliyeipandisha timu hiyo baada ya kutupiwa virago na Polisi Tanzania msimu uliopita.

Licha ya Malale kutoweka bayana wachezaji waliotua katika kikosi hicho, lakini tetesi zinadokeza kuwa walisajiliwa hadi sasa ni Danny Lyanga, Deusdedith Okoyo na George Wawa kutoka Geita Gold, Ismail Aziz Kader aliyetoka Azam FC na Hassan Dilunga aliyeachana na Simba SC.

Chanzo: Dar24