Yanga itaikarbisha JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Bara Agosti 29 katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi saa 1:00 usiku
Yanga ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi tatu katika mechi sawa na JKT Tanzania ambayo ipo nafasi ya Sita
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi akizuungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam na amesema wamejiandaa vizur katika mchezo huo na anataka mabao ili kuwafurahisha Wananchi
“Licha ya kwamba mpinzani wetu tunajua ni timu iliyopanda daraja, najua kwamba wana wachezaji wenye uzoefu kwenye ligi hivyo hatupaswi kuichukulia kama timu dhaifu au ngeni kwenye ligi"
"Ni wageni kwa maana ya timu lakini wana idadi kubwa ya wachezaji wenye uwezo lakini sisi ni timu kubwa na tupo nyumbani nafikiri kesho tunapaswa kujiamini na kufunga magoli mengi" amesema Gamondi
Kwa upande wake kocha msaidizi wa JKT Tanzania George mketo amesema amejiandaa vizuri na mchezo wa kesho kwa asilimia 90 kikosi chake kipo sawa Ila hatishwi na matokeo ambayo mpinzani wake ameyapata hivi karibuni
"Tumejiandaa vizuri, Yanga ni timu kubwa tunawaheshimu, kikosi changu kwa asilimia 90 kipo sawa na tumejipanga kupata matokeo mazuri"
"Tunajua mpinzani wetu amekuwa akipata matokeo mazuri kwenye michezo ya hivi karibuni hilo sisi halitutishi kwani alicheza na timu nyingine na sio JKT Tanzania"
Yanga katika mchezo wake waufunguzi Ligi Kuu aliichapa KMC mabao 5-0 katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi huku JKT Tanzania alishinda mechi ya dhidi ya Namungo kwa bao 1-0