Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKT Tanzania waichapa Tabora United Chamazi

JKT Tanzania.jpeg JKT Tanzania waichapa Tabora United Chamazi

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya JKT Tanzania imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex Jijini Dar es Salaam.

Bao pekee la JKT Tanzania ambayo Tabora United zote zimepanda Ligi Kuu msimu huu limefungwa na kiungo na Maka Edward Mwasomola dakika ya 17.

Kwa ushindi huo, JKT Tanzania ambao ni mabingwa wa Ligi ya Championship msimu uliopita inafikisha pointi 11 na kusogea nafasi ya tano, wakati Tabora United inayobaki na pointi zake tisa inaangukia nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi saba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live