Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKT Tanzania sio kipimo sahihi kwa Yanga?

YANGA NZENGELI.jpeg JKT Tanzania sio kipimo sahihi kwa Yanga?

Wed, 30 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukiona Shabiki wa Yanga anatembea anacheka cheka njiani, mwache tu, anafanya review ya utamu alioushuhudia Azam Complex, Chamazi what a football from the boys.

Natamani kusema JKT Tanzania sio kipimo sahihi kuupamba ubora wa Yanga lakini nikikumbuka namna walivyozuia first half nakaa kimya, walikua solid sana, waliminya mianya ya mipira kupita kwenye half spaces, zuia nafasi ya Max na Aziz Ki kupokea mipira kwenye maeneo finyu na kupiga killer pass niliamini wamefanikiwa hadi pale waliporuhusu bao la kwanza.

Moja ya vitu vitakavyowatesa wengi ni tank la mafuta la wachezaji wa Yanga kuanzia dakika ya kwanza mpaka 90, muda ambao wewe unachoka wao ndo kwanza wanaanza mechi, kama ni mtu anakudai anakuja vile kwako kila wakati ni heri ukamkopee pesa yake sehemu nyingine umpe.

Max Nzengeli anakuja, Aziz Ki anakusubiri kwenye nafasi, huku Mudathir anakuja pembeni Kibabage na Yao wanakuja wakati huo Aucho kafanya utawala dimba la kati, utachagua wewe nani umkabe kila mtu anafunga lakini sio wote.

Ni onyo kali kwenda Chamazi Complex kucheza na Yanga kama tank lako la mafuta lipo nusu, adhabu yake ni mabao yasiyopungua matano Wamedhamiria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live