Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKT Tanzania sasa kazi ni kubaki Ligi Kuu

JKT Tanzaniaaaaa JKT Tanzania sasa kazi ni kubaki Ligi Kuu

Tue, 9 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, JKT Tanzania imesema kwa sasa wanaelekeza nguvu Ligi Kuu ili kupambania timu hiyo kutoshuka daraja.

Maafande hao hawana matokeo mazuri wakiwa nafasi mbili za mkiani kwa pointi 20 katika Ligi Kuu, ambapo wanatarajia kuwa uwanjani Aprili 14, kuwakabili Tabora United.

Timu hiyo ikicheza juzi mechi ya Kombe la Shirikisho hatua ya 16, ilitupwa nje baada ya kutolewa dhidi ya Coastal Union kwa penalti 5-4 kufuatia suluhu ya bila kufunga katika dakika 90.

Nahodha wa timu hiyo, Nurdin Mohamed alikiri matokeo kutokuwa mazuri akieleza kuwa walitamani kufika mbali lakini kuondolewa kwao Kombe la Shirikisho inawafungulia mlango wa Ligi Kuu.

Alisema kwa sasa ni muda wa kila mchezaji kuwa siriasi kuipambania timu hiyo kukwepa aibu ya kushuka tena daraja, akifafanua kuwa kupanda Ligi Kuu si kazi nyepesi.

“Tulipambana lakini haikuwa bahati yetu hadi kuondolewa kwa penalti, ila hatukati tamaa bali kujipanga sasa na michezo ya Ligi Kuu ili kubaki salama, matokeo si mazuri sana,” alisema Nurdin.

Beki huyo aliongeza kuwa makosa yaliyoonekana benchi la ufundi litafanyia kazi, lakini hata wachezaji wenyewe watakaa na kujisahihisha pale walipokosea kwenye michezo iliyopita.

“Bado tuna matumaini kwa sababu walio juu yetu pointi tunaweza kuzifikia au hata kuzipita, kimsingi ni kila mmoja kutimiza wajibu ili kujinasua nafasi za chini” alisema staa huyo.

Chanzo: Mwanaspoti