Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKT Tanzania kuingia sokoni Dirisha Dogo

JKT Tanzania.jpeg JKT Tanzania kuingia sokoni Dirisha Dogo

Thu, 21 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Malale Hamsini amesema timu yake inapoteza mechi mbalimbali za Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na Walinda Lango wake kufungwa mabao ya kizembe, hivyo analazimika kuingia sokoni kusaka nyota wapya watakaongeza nguvu katika kikosi chake.

Malale amesema anaamini ujio wa Walinda Lango wapya utasaidia kuwapa changamoto Walinda Lango waliopo na hivyo kuisaidia timu kupata matokeo mazuri.

Kocha huyo amesema mara kwa mara timu yake imepoteza mechi za Ligi Kuu Bara kwa kufungwa mabao mepesi kutokana na Walinda Lango wake kufanya makosa ambayo yanazuilika.

“Ninatarajia kuingia sokoni katika Dirisha Dogo la usajili kusaka wachezaji wengine, pamoja na mambo mengine nitashusha kipa mwingine kwa ajili ya kuleta changamoto,” amesema Malale

Ameongeza katika mechi dhidi ya Azam FC kulikuwa na makosa ambayo yalisabisha waruhusu aina fulani ya mabao, lakini hali hiyo ilijirudia Jumatatu iliyopita walipocheza dhidi ya Coastal Union, na kufungwa bao 1-0.

“Tumefungwa goli jepesi, langoni kipa wetu anashindwa kuisaidia timu, kazi kubwa ya mwalimu ni kuwaelekeza wachezaji jinsi ya kutengeneza nafasi, lakini kuingiza mpira ndani ya wavu ni ya mchezaji mwenyewe, utaona tumetengeneza nafasi nyingi, lakini mtu yeye na kipa au na wavu anashindwa kufunga, halafu sisi tunafungwa bao rahisi vile, amesema kocha huyo.

Tayari Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), limeshafungua dirisha dogo la usajili na litafungwa rasmi Januari 15, mwakani na kalenda hiyo inazihusu timu zote za zinazoshiriki Ligi Kuu Bara, Ligi ya Championship. First League na Ligi Kuu Wanawake ambayo ilianza kwenye viwanja mbalimbali jana jumatano (Desemba 20).

JKT Tanzania inashika nafasi ya tisa katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 16 baada ya kucheza michezo 14.

Chanzo: Dar24