Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKT, Tabora kumalizana kibabe Dar

Jkt Tzzzzz JKT Tanzania

Sat, 8 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maafande wa JKT Tanzania jioni ya leo watakuwa na kibarua cha kujihakikishia kubaki Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao wakati watakapoikaribisha Tabora United katika pambano la marudiano la play-off huku wakiwa na hazina ya ushindi wa mabao 4-0 walioupata ugenini mwanzoni mwa wiki hii.

Timu hizo zilizopanda daraja msimu huu na kujikuta zikiangukia kwenye play-offs zitavaana kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, baada ya Jumanne iliyopita kuvaana kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na wenyeji ‘Nyuki’ kukubali kichapo cha mabao 4-0 na sasa inalazimika leo kushinda zaidi ya mabao hayo ili isalie Ligi Kuu.

Mshindi wa jumla wa mechi hiyo atajihakikisha kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao na timu itakayopoteza itaenda kucheza na Biashara United ya Ligi ya Championship ili kusikilizia kama itasalia na kushuka daraja kuipisha Biashara iungane na KenGold na Pamba Jiji zilizotangulia mapema Ligi Kuu kwa msimu wa 2024-2025.

Wachezaji na makocha wa timu zote wametambiana mapema kila mmoja akiamini watapata ushindi na kutimiza ndoto za kubaki Ligi Kuu Bara.

Kocha wa JKT, Malale Hamsini alisema haitakuwa mechi rahisi baada ya kuwafunga Tabora kwao, kwani watashuka Isamuhyo wakiwa na hasira, lakini wamejiandaa kukamilisha pale walipoishia katika mechi ya kwanza.

Tabora inashuka uwanjani ikiwa na kocha msaidizi, Benny Fabian baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa mpito, Masoud Djuma kutemwa kutokana na matokeo mabaya iliyokuwa nayo timu hiyo, huku akinukuliwa akisema wachezaji wapo tayari kupambana hadi dakika ya mwisho kuiokoa Tabora isirudi ilikotoka.

Tabora na JKT Tanzania ni kati ya timu tatu zilizopanda daraja msimu ulioisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live