Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKT TZ yazidi kuzamisha jahazi la Mtibwa Ligi Kuu

JKT TZ VS Mtibwa Sugarr JKT TZ yazidi kuzamisha jahazi la Mtibwa Ligi Kuu

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, JKT Tanzania wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jana Jumatatu Uwanja wa Meja Mstaafu Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya JKT Tanzania yamefungwa na Edson Katanga dakika ya saba na Sixtus Sabilo dakika ya 90, wakati bao pekee la Mtibwa Sugar limefungwa na Charles Ilamfya dakika ya 22.

Kwa ushindi huo, JKT Tanzania inafikisha pointi 26 katika mchezo wa 24 na kusogea nafasi ya 10, wakati Mtibwa Sugar inabaki nafasi ya mwisho kwenye Ligi ya timu 16 ikiwa na pointi 17 za mechi 23 sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: