Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKT Queens yaanza vibaya CAF

JKT Queens 2023 JKT Queens yaanza vibaya CAF

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa ya Wanawake JKT Tanzania imeanza vibaya michuano hiyo baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Mamelodi Sundowns kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi uliochezwa jana Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly, Ivory Coast

Mabao la Mamelodi yamefungwa na Lebohang Ramal dakika ya 40 ya mchezo na kipindi cha pili wakapata bao la pili dakika ya 74 Refilwe Tholakele 75.

Mchezo huu ni wa kwanza kwa JKT Queens kukutana na Mamelodi na pia hii inakuwa mara ya pili kwa timu za Tanzania kushiriki michuano hiyo baada ya msimu uliopita Simba Queens kuchukua ubingwa wa CECAFA na kuishia nusu fainali CAF.

Michuano hii imeanza jana Novemba 05 na JKT wanakibarua kingine Novemba 08 saa 2 usiku dhidi Atlentico Abidjan ya Ivory Coast na kumaliza na SC Casablanca ya Morocco Novemba 11 hatua ya makundi ambapo timu hiyo imepangwa kundi A.

Chanzo: Mwanaspoti