Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKT Queens wamchapa mwenyeji Ligi ya Mabingwa

JKT Queens Vs Abdijan Kikosi cha JKT Queens

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi wa CECAFA katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa kwa upande wa Wanawake (CAFWCL) JKT Queens imepata ushindi wa wake wa kwanza wa mabao 2- 1 dhidi ya Atletico Football Club d'abidjan ya Ivory Coast.

Mabao ya Aliyah Fikiri na Winifrida Gerald yameifanya JKT Queens kukusanya alama tatu katika michezo miwili waliyocheza ambapo walipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Kwenye mchezo wa leo Donisia Minja amekuwa mchezaji Bora wa mechi (women of the match).

Hata hivyo JKT Queens atatakiwa kushinda mchezo ujao dhidi ya Sporting Casablanca mchezo utakaochezwa Novemba 11 ili kujihakikishia nafasi ya kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live