Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKT Queens ni mahesabu tu kubeba Ubingwa

JKT Queens JKT Queens

Sat, 8 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya JKT Queens wamesema baada ya kukaa kileleni hawatoki na wanadeni katika mechi tano walizobakisha za Ligi Kuu ya Wanawake (WPL), kuhakikisha zote wanashinda.

Mabingwa hao mara mbili wa ligi hiyo, wanaongoza msimamo mara baada ya juzi kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ceasiaa Queens ya mkoani Iringa katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Meja General Isamuhyo mkoani Dar es Salaam.

Katika mchezo huo mabao ya JKT Queens yalifungwa na Stumai Abdallah na Zabela John, hivyo kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo wowote mpaka sasa.

Timu hiyo imebakiza michezo mitano, minne ugenini dhidi ya Amani Queens (Ilulu) Yanga Princess (Uhuru), Fountian Gate Princess (Jamhuri), Mkwawa Queens (Chuo cha Mkwawa) na nyumbani mmoja dhidi ya Amani Queens (Meja General Isamuhyo).

Kocha wa timu hiyo, Ally Ally alisema baada ya kukaa kileleni hawatarajii kutoka kwani wamejipanga kushinda michezo yote mitano iliyobaki.

“Huku juu hatutoki tena na tutahakikisha tunashinda michezo yetu yote iliyobaki ina maana tukishinda sisi ndio mabingwa hatutaki kukosea tunajipanga kuhakikisha tunashinda michezo hiyo,” alisema kocha huyo.

Kuhusu mchezo dhidi ya Ceasiaa Queens alisema: “ Ulikuwa mgumu tulipata mabao ya haraka haraka kipindi cha kwanza, kipindi cha pili tukarudi kuyalinda tunashukuru tumepata matokeo tunajipanga kwa michezo inayofuata."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live