Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKT Queens kujichimbia Uholanzi

JKT Quens Bungeni JKT Queens kujichimbia Uholanzi

Sat, 17 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa JKT Queens, Ally Ally amesema kikosi hicho kitakwenda nchini Uholanzi kushiriki mashindano ya wiki mbili ya timu za majeshi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maafande hao na Ligi ya Mabingwa Ukanda wa CECAFA.

Mashindano hayo yanayotarajia kufanyika kati ya Agosti 12 hadi 26, mwaka huu nchini Uganda ambapo JKT Queens inaiwakilisha nchi baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara msimu huu.

JKT Queens iliivua ubingwa Simba Queens ambayo iliushirikia ubingwa huo kwa misimu mitatu mfululizo na kama watatwaa ubingwa wa CECAFA basi watauwakilisha ukanda huo kwenye

Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake. Akizungumza na Mwanaspoti, Ally ambaye amedumu klabuni hapo kwa zaidi ya misimu mitatu alisema wataondoka nchini kati ya Juni 25 na 26, mwaka huu kwenda Uholanzi.

“Tunakwenda na timu hii ya wanawake (JKT Queens) kwenye mashindano ya majeshi huko Uholanzi ni mashindano ya wiki mbili kwahiyo ndiyo tuko kwenye maandalizi hayo kwa sasa tukirudi ndiyo tutaendelea na maandalizi mengine ya CECAFA,” alisema Ally

Katika hatua nyingine, Ally amefunguka juu ya tetesi za kutemwa na maafande hao na nafasi yake kupewa kocha wa timu za taifa, Bakari Shime, ambapo alisema; “Mimi bado ni kocha mkuu JKT Queens na hakuna kocha mwingine aliyetangazwa hadi sasa kuwa kocha mkuu, na kuhusu timu ya taifa ya wanawake sijachaguliwa ila nillienda safari kwa ajili ya kupata uzoefu wa mechi za kimataifa,”

“Kumekuwa na hofu kuhusu vyeti vinavyohitajika na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwenye ligi ya mabingwa nadhani hilo viongozi wangu wanalifanyia kazi kila kitu kitakuwa sawa na mtapewa majibu,” alisema

Chanzo: Mwanaspoti