Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKT Queens kuanza na Mamelodi Klabu Bingwa

Jkt Queens Gf.jpeg JKT Queens kuanza na Mamelodi Klabu Bingwa

Sun, 15 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Bingwa Afrika, JKT Queens imepewa kuanza kuvaana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwenye mechi ya Kundi A, mchezo utakaochezwa Novemba 5, saa 11:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Shirikisho la Soka Afrika, limeachia ratiba hiyo ya Ligi hiyo ya soka ya Wanawake yatakayoanza kutimua vumbi Novemba 5 hadi 19.

Mechi ya JKT Queens ni ya pili katika ufunguzi huku ya kwanza ikiwa ni Atletico Abidjan dhidi ya Sporting Club Casablanca mchezo utakaochezwa saa 8:00 mchana katika uwanja wa Korhogo's Stade Ahmadou Gon Coulibaly.

Baada ya mchezo huo JKT Queens itacheza mchezo wake wa pili dhidi ya Atletico Abidjan, Novemba 8 saa 8:00 mchana kisha itamalizia dhidi ya Sporting Club Casablanca mchezo utakaochezwa Novemba 11 saa 12:00 jioni.

Baada ya hatua hiyo mshindi wa kwanza katika kundi A atacheza na mshindi wa pili katika kundi B katika robo fainali ya kwanza na robo fainali ya pili atacheza mshindi wa kwanza kundi B dhidi ya mshindi wa pili kundi A.

JKT imepata nafasi hiyo baada ya kutwaa ubingwa wa Ukanda wa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) iliyofanyika Uganda na inakuwa klabu ya pili ya Tanzania kucheza fainali hizo baada ya Simba Queens iliyoshiriki msimu uliopita na kumaliza ya nne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live