Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ivory Coast yasubiri rekodi miaka 18

Ivory Coastre Ivory Coast yasubiri rekodi miaka 18

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya Ivory Coast kutinga fainali ya Afcon, hivi sasa ina mtihani mgumu wa kuhakikisha inatwaa ubingwa tofauti na mataifa mengine yaliyoandaa fainali hizo kwa miaka ya hivi karibuni ambayo yaliishia njiani katika safari hiyo ngumu.

Juzi, Ivory Coast iliingia fainali ya michuano hiyo mikubwa Afrika kwa soka barani Afrika baada ya kuichapa DR Congo kwa bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali na sasa inatarajiwa kukutana na Nigeria ambayo iliipiga kikumbo Afrika Kusini kwa penalti 4-2 baada ya sare ya bao 1-1 katika dakika 120.

Mshambuliaji Sebastien Haller anayeichezea Borrusia Dortmund ya Ujerumani, ambaye hakuwa na kiwango bora kwenye michezo kadhaa iliyopita aliifungia timu hiyo bao pekee kwenye mchezo huo katika dakika ya 65, lililopeleka majonzi DR Congo, moja ya timu pekee kutoka Afrika Mashariki iliyokuwa imebaki katika mashindano hayo baada ya Tanzania kutolewa.

Ivory Coast ambao ni mabingwa mara mbili wa michuano hiyo wamekuwa timu ya kwanza kuandaa michuano hiyo na kutinga fainali tangu 2006 ambapo Misri walifanya hivyo na kutwaa ubingwa.

Hii inaonyesha kuwa sasa timu hiyo inatakiwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Nigeria ambayo imetwaa ubingwa wa michuano hiyo mara tatu ili kuweka rekodi mpya baada ya miaka 18 iliyopita ya waandaaji wa michuano hiyo.

Chanzo: Mwanaspoti