Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ivory Coast yaimarisha ulinzi AFCON 2023

African Cup Of Nations 2023.png Ivory Coast yaimarisha ulinzi AFCON 2023

Sat, 23 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Kuelekea Fainali Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ nchini Ivory Coast waandaaji wana imani hatua za kiusalama zinazochukuliwa zitazuia kujirudia kwa vurugu zilizogubika mashindano ya mwaka 2021 nchini Cameroon.

Ivory Coast inaweza kuwa moja ya timu zenye uzito mkubwa katika soka la Afrika lakini hii itakuwa mara ya pili kuwa wenyeji wa fainali hizo, baada ya mwaka 1984 ambapo mashindano hayo yalishirikisha timu nane tu badala ya 24 wakati huu.

Mashindano hayo yanaanza Januari 13 hadi Februari 11, mwakani huku Senegal wakitetea taji waliloshinda kwa mara ya kwanza baada ya kuifunga Misri kwa Penati.

Inabakia kuwa shindano la 2023 licha ya uamuzi wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) Julai mwaka jana kuiahirisha kutoka tarehe za awali katika majira ya joto ya Kaskazini kutokana na hofu juu ya msimu wa mvua.

Karibu Dola Bilioni 1.5 zimewekezwa ambazo ni pamoja na kufadhili barabara zilizoboreshwa hasa barabara ya Pwani ya Kilomita 350 inayounganisha Abidjan mji mkuu wa kiuchumi na mji wa bandari wa San Pedro na kukata nusu ya muda wa kusafiri kati ya miji hiyo miwili.

Mbali na hatari ya usalama wa nje inayosababishwa na wapiganaji wa jihadi wanaoishi katika nchi jirani za Mali na Burkina Faso, mamlaka za Ivory Coast zimechukua hatua ya kutuliza hofu juu ya udhibiti wa umati wa watu ambao umekuwa chanzo cha wasiwasi mkubwa kutokana na kile kilichotokea Yaounde miaka miwili iliyopita.

Mchezo wa mwisho wa 16 kati ya wenyeji Cameroon na Comoro ulisababisha vifo vya watu wanane na wengine kadhaa kujeruhiwa kutokana na purukushani wakati mashabiki wa Cameroon wakimiminika kutazama mechi hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Polisi wa Ivory Coast, Youssouf Kouyate, amesema wana mikakati ya kuzuia janga kama hilo huku waandaaji wakitarajia mashabiki milioni 15 kutoka nje ya nchi.

“Tutafungua milango mapema sana, tutahakikisha watazamaji wanatengeneza foleni ya utaratibu ili waweze kuingia uwanjani bila shida yoyote,” alisema.

“Tutataka watazamaji waje mapema. Kutakuwa na Wanajeshi 17,000 na Polisi kwa ajili ya mashindano hayo na Wafanyakazi 2,500 wa uwanja.

“Ni baada ya yote sio tukio kubwa la kwanza la michezo Ivory Coast imelazimika kujipanga. Tulishiriki michezo ya Kifaransa (mwaka 2017). Sisi ni watulivu.” alisema Kouyate.

Chanzo: Dar24