Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ivory Coast yachezea kipigo kizito nyumbani

Ivory Coast Zdc Ivory Coast yachezea kipigo kizito nyumbani

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya Equatorial Guinea imewashangaza wengi jana Jumatutu, Januari 22, 2024 ilipoweka historia katika Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, kwa kuwalaza wenyeji Ivory Coast, mabao manne kwa nunge na kushinda katika Kundi A, na hivyo kutinga hatua ya 16 bora.

Katika hatua ya mtoano Nigeria wameibuka nafasi ya pili Kundi A, huku washindi Cape Verde wakiibuka vinara kundi B, wakiungana na mabingwa mara saba wa kinyang’anyiro hicho, Misri, kwenye hatua inayofuata.

Nigeria waliwafunga Guinea-Bissau 1-0, na kumaliza wakiwa wa pili nyuma ya Equitorial Guinea, huku sare ya 2-2 kati ya Cape Verde na Misri, ikiruhusu timu hizo kusonga mbele.

Ghana ilipigwa mabao mawili katika muda wa ziada na kutoka sare ya 2-2 na Msumbiji, na, ikiwa na pointi mbili pekee, huenda isiwe miongoni mwa timu nne bora zilizo katika nafasi ya tatu ambazo pia zitafuzu.

Leo Jumanne, Gambia watapambana na Cameroon, huku Guinea Conakry wakimenyana na Senegal, wakati Mauritania nao wakionyeshana kivumbi na Algeria, ambapo baadaye, Angola na Burkina faso wataingia uwanjani kutoana jasho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live