Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ivory Coast walikuwa hawamtaki kocha wale

Ivory Coast ADaG1.jpeg Mabingwa wa Afcon 2023, Ivory Coast

Sat, 17 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hapa Afrika kama kocha hatakiwi kwenye timu iwe na viongozi au wachezaji ni jambo rahisi sana kulifahamu kwani ishara ziko nyingi.

Na ishara mojawapo huwa ni kubadilika kwa ghafla kwa timu namna inavyocheza mara baada ya kutoka kufanya vibaya na utaiona inaanza kufanya vizuri.

Nyingine ni aina ya kikosi kinachopangwa na kocha mpya au yule anayekaimishwa usimamizi wa benchi la ufundi baada ya kocha wa mwanzo kuondoka ambapo utaona wachezaji waliokuwa hawapewi nafasi na kocha wa zamani wanapangwa na kocha mpya.

Naweza kuichukulia timu ya taifa ya Ivory Coast iliyotwaa ubingwa wa Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 zilizofanyika mwaka huu huko kwao kama mfano tosha wa hilo.

Jamaa walicheza ovyo sana katika hatua ya makundi na kujikuta wakishinda mechi moja na kupoteza mbili kati ya tatu, ikiwamo waliyokula kipigo kikubwa katika historia yao cha mabao 4-0 kutoka kwa Equitorial Guinea, jambo lililowaweka katika hatari ya kutolewa mashindanoni.

Wakachukua uamuzi mgumu wa kumfukuza kocha wao mkuu Jean-Louis Gasset na kumpa kibarua cha kuinoa timu hiyo kocha msaidizi Emerse Fae ambaye alikuja kuiongoza timu hiyo hadi ikatwaa ubingwa baada ya kuingia hatua ya 16 bora kwa tiketi ya timu shindwa zilizofanya vizuri (Best Losers).

Jamaa baada ya kupewa timu, kwanza alifanya mabadiliko ya kikosi kwa kuwapa nafasi wachezaji waandamizi ambao mtangulizi wake alikuwa akiwatupa benchi kwenye makundi.

Ndani ya uwanja timu ilionekana kubadilika na kucheza kwa kujituma vilivyo tofauti na ilivyokuwa na kocha wa zamani huku wachezaji waandamizi kikosini wakiongoza kwa vitendo.

Inaonekana kama Gasset alishachokwa na Ivory Coast kwani kama suala lingekuwa ni ubora wa wachezaji, isingekuwa rahisi timu hiyo ionyeshe kiwango bora namna ile hadi kutwaa ubingwa baada ya yeye kuondoka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live