Waandaaji wa kombe la Afcon 2023 Ivory Coast watategemea matokeo mengine ili kuzuia kuondolewa katika michuano hiyo katika kundi lao baada ya Equitoriol Guinea kuwacharaza ndovu hao 4 – 0 mjini Abidjan.
Mabao mawili ya Emilio Nsue, mkwaju wa faulo wa umbali wa yadi 25 wa Pablo Ganet na bao la dakika za lala salama la Yannick Buyla yaliipa National Thunder ushindi maarufu na kutinga kileleni katika Kundi A.
Wenyeji lazima watoe jasho katika kufuzu baada ya kushika nafasi ya tatu kwenye kundi.Timu nne bora zilizo katika nafasi ya tatu katika makundi sita zinafuzu hadi 16 bora.
Ibrahim Sangare mara mbili alisababisha mabao ya kusawazisha ambayo yalikataliwa upande wa Ivory Coast walipokuwa nyuma kwa bao pekee, lakini Tembo walipoteza nafasi nyingi na wakalazimishwa kulipa na upinzani.
Baadhi ya wachezaji wa Ivory Coast walikuwa wakibubujikwa na machozi kwenye filimbi ya mwisho walipozomewa kwa sauti na umati wa watu wenye hasira kwenye Uwanja wa Alassane Ouattara baada ya moja ya maajabu makubwa katika historia ya Afcon.
Kikosi cha Equatorial Guinea, kilisherehekea kwa fujo baada ya kuandikisha ushindi mwingine wa kishindo kwenye fainali hizo na watamenyana na timu iliyoko katika nafasi ya tatu kutoka Kundi C, D, au E katika hatua ya 16 bora Jumapili.
Uchezaji wao bora katika michuano ya Afcon ulikuwa kufikia nusu fainali kama wenyeji mwaka wa 2015 lakini walimaliza juu ya mabingwa mara tatu Nigeria na Ivory Coast, washindi mara mbili, katika hali isiyotarajiwa.
Ivory Coast italazimika kusubiri makundi mengine yote kumaliza siku ya Jumatano ili kuona kama pointi zao tatu na tofauti ya mabao -3 inatosha kutinga hatua ya muondoano.