Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ivory Coast ilivyowashangaza kina Inonga

Ivory Coastre Ivory Coast ilivyowashangaza kina Inonga

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikishuhudiwa na nyota wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba, timu ya Taifa ya Ivory Coast imefuzu fainali ya Afcon baada ya kuifunga DR Congo bao 1-0, kwenye Uwanja wa Alassane Ouattara.

Bao la ushindi la Tembo hao lilifungwa na Sebastian Haller dakika ya 68, akiunganisha krosi safi ya Max Gradel mpira uliompita kipa wa Congo, Lionel Mpasi-Nzau na kutinga nyavuni.

Ivory Coast ambao walifuzu hatua ya mtoano (16 bora), ikiwa 'best looser' imeonyesha soka safi huku nyota wa zamani wa timu hiyo Drogba akipata mzuka wakati miamba hiyo ikitinga fainali.

Haller anayekipiga klabu ya Borussia Dortmund alionyesha ubora wake huku akikosa baadhi ya mabao lakini bao hilo alilifunga kiufundi, lilitosha kuifanya Abidjan kulipuka kwa shangwe za mashabiki waliofurika uwanjani hapo.

Nyota wa Simba, Henock Inonga na Fiston Mayele aliyetamba akiwa na Yanga misimu miwili iliyopita wamejikuta akibubujikwa na machozi baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya mwisho, sasa watacheza mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu dhidi ya Afrika Kusini iliyofungwa kwa penalti 4-2 na Nigeria katika mchezo wa kwanza uliopigwa kuanzia saa 2:00 usiku kwenye Uwanja wa Bouake.

Kutinga fainali kwa Ivory Coast kunaifanya ikasake taji la tatu la michuano hiyo inayofanyika nchini kwao baada ya awali kutwaa mwaka 1992 na 2015.

Ilianza kwa kusuasua baada ya ushindi wa mechi ya kwanza dhidi ya Guinea Bissau mabao 2-0, kabla ya kufungwa bao 1-0 na Nigeria ambao itakutana nao kwenye fainali.

Mchezo wa tatu hatua ya makundi ikiwa kundi A, ilipata kichapo cha mabao 4-0 na kusababisha mashabiki wa timu hiyo kuzua vurugu huku wakiikatia tamaa timu yao hiyo.

Kitendo cha kumaliza nafasi ya tatu na pointi tatu ziliisaidia timu hiyo kufuzu 16 bora kama best looser na ilikutana na Senegal na kuiondoa kwa mikwaju 5-4 baada ya dakika 120, za kawaida 90 na nyongeza 30 kutoka sare ya bao 1-1.

Tembo hao walitinga robo fainali na ilikutana na Mali na kuifunga mabao 2-1 na kutinga nusu fainali iliyokutana na DR Congo.

Mchezo wa fainali utapigwa Februari 11 kwenye Uwanja wa Alassane Ouattara jijini Abidjan baada ya mchezo wa mshindi wa tatu wa Afrika Kusini dhidi ya DR Congo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live