Klabu ya Brentford imesisitiza inahitaji zaidi ya Pauni 80 Milioni ili kumuuza Mshambuliaji lvan Toney, ambaye Arsenal na Tottenham zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili katika dirisha la majira ya baridi Januari mwakani.
Toney mwenye umri wa miaka 27, kwa sasa anatumikia kufungo cha Chama cha Soka cha England ‘FA’ baada ya kukutwa na hatia ya kujihusisha na Kamari, ifikapo wakati huo kifungo chake kitakuwa kimemalizika.
Timu zote zilivutiwa na kiwango cha staa huyu alichoonyesha kabla hajafungiwa msimu uliopita alicheza mechi 35 za michuano yote, kufunga mabao 2 l na kutoa asisti tano.
Tottenham inamuangalia straika huyo kama mbadala wa Harry Kane wakati Arsenal inamataka kama mbadala wa Gabriel Jesus ambaye amekuwa na majeraha ya mara kwa mara.
Mkataba wa sasa wa mshambuliaji huyo unatarajiwa kumalizika mwaka 2025. Spurs imepanga kutumia pesa iliyopata baada ya kumuuza Kane kwenye kukamilisha uhamisho wake.