Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Italia yamkomalia De Gea

David De Gea Record David De Gea

Sun, 28 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Italia, Genoa ni moja kati ya timu zilizowasilisha ofa kwa wawakilishi wa kipa wa zamani wa Manchester United, David de Gea ili kumsajili katika dirisha hili la majira ya kiangazi ambalo yupo huru.

De Gea ambaye ana umri wa miaka 33, amedhamiria kurudi uwanjani kwa msimu ujao na hadi kufikia sasa timu kibao kutoka Saudi Arabia, Marekani na Italia zimeonyesha nia ya kumsajili.

Genoa inahitaji huduma ya kipa huyu kwa ajili ya kuziba pengo la Josep Martinez aliyeuzwa kwenda Inter Milan katika dirisha hili.

Kocha wa Genoa, Alberto Gilardino anaamini kwamba De Gea anaweza kuwa kiongozi mzuri katika safu ya ulinzi kutokana na uzoefu wake na hiyo itawawezesha kufikia malengo yao ya kumaliza ndani ya nafasi 10 za juu kwa msimu ujao baada ya kumaliza katika nafasi ya 11 msimu uliopita.

Mbali ya Genoa, De Gea anawindwa na timu za Saudia hususani Al Nassr lakini inadaiwa hana mpango wa kwenda huko licha ya kiasi kikubwa cha pesa walichomwekea mezani.

Kwa mujibu wa ripoti, Al Nassr ambayo inapambana kupata kipa kutoka katika zile ligi tano kubwa barani Ulaya, ilimwekea De Gea mshahara unaofikia Pauni 500,000 kwa wiki.

Ukiondoa Al Nassr, kule Marekani huduma ya kipa huyu raia wa Hispania inawindwa na timu ya Lionel Messi, Inter Miami.

De Gea ambaye amekuwa nje ya uwanja kwa msimu mzima tangu alipoachana na Man United katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana baada ya kuitumikia kwa karibu miaka 12, na sasa anafanya mazoezi yake binafsi akijiandaa na katika kutua timu atakayokubaliana nayo katika dirisha hili.

Akiwa United aliichezea mechi 545.

Chanzo: Mwanaspoti