Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Italia kuna mtu atalia siku ya mwisho

Inter Milan Are Crowned 2023 24 Serie A Champions  Besoccer.png Italia kuna mtu atalia siku ya mwisho

Mon, 20 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Imebakia mechi moja tu kabla ya msimu huu wa Ligi Kuu Italia (Serie A) kumalizika huku msimamo ukionyesha kwamba kuna mashabiki wanaweza kuangusha machozi katika siku ya mwisho ya ligi hiyo.

Hii ni kutokana na msimamo ulivyo kule chini, tayari Sassuolo na Salernitana zimeshashuka daraja lakini inatakiwa timu moja ya kuungana nazo.

Hadi sasa Empoli ndio inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kuungana nazo lakini mambo yanaweza kubadilika siku ya mwisho.

Empoli ambayo ipo katika nafasi tatu za mwisho ikishikilia namba 18 kwa pointi 33, ikiwa itashinda mechi yao ya mwisho dhidi ya Roma itafikisha pointi 36 ambazo zinaweza kuwawezesha kuivuka timu moja kati ya tatu zilizo juu yake aidha Udinese, Verona au Frosinone.

Tofauti ya alama kati yao na Udinese na Verona ni moja wakati Frosinone zikiwa ni tatu, hivyo timu moja kati ya hizi ikipoteza ama kupata sare kisha Empoli ikashinda, rasmi watakuwa wamesalia Ligi Kuu msimu ujao.

Bahati nzuri kwa Empoli ni kwamba mechi ya mwisho ya Verona itakutana na mabingwa Inter Milan hivyo kuna uwezekano mkubwa ikaangusha alama lakini wao pia wana mchezo mgumu dhidi ya Roma.

Pia machozi yanaweza kumwagika kwa mashabiki wa timu mbili kati ya Fiorentina, Napoli ama Torino ambao timu zao zinagombania kufuzu Uefa Conference League.

Hadi sasa Fiorentina ndio ipo katika nafasi hiyo ya nane ikiwa na pointi 54, ikifuatiwa na Torino yenye pointi 53 pamoja na Napoli yenye alama 52.

Jambo zuri kwa Fiorentina ni kwamba ina kiporo cha mchezo mmoja mkononi dhidi ya Atalanta ambacho watacheza Juni 02, kutokana na jukumu la Atalanta la kuipambania Italia katika michuano ya Europa League ambapo ipo hatua ya fainali na itacheza dhidi ya Beyer Leverkusen Mei 22.

Chanzo: Mwanaspoti