Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Italia: Wachezaji Watakaopinga Chanjo Hawataruhisiwa Kucheza

Serie A 2021 22 Ligi Kuu ya Seie A

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Italia, waziri wa Afya wa amethibitisha wachezaji wote wanaopinga chanjo na wasiotaka kuchanjwa hawataruhusiwa kucheza tena, huku akiibua maswali kwa timu za nje zitakazo kuja kucheza nchini humo.

Tamko hilo la serikali leo limepitishwa na linatarajiwa kuanza kufanya kazi kuanzia 2 January, baada ya wimbi la nne la kirusi cha Omicron kusambaa kwa kasi, pia idadi ya mashabiki watakao ruhusiwa kuingia uwanjani imepunguzwa kutoka asilimia 75 hadi 50 pia watakao ruhisiwa ni wale tu waliochanja.

“Wachezaji ambao hawatachanja hawaturusiwa kucheza tena msimu huu, milipuko imekuwa ikibadilika na hatuwezi kuwatoa sadaka kama iliyotuka miaka miwili ilyopita, tumetoa ufafanuzi kuhusu tanko la serikali, tusisahau kuwa kumi kati ya nane waliolazwa hospitali ni watu wasiochanja.” Alisema waziri wa afya

kwenye ligi kuu ya italia serie A asilimia 98 ya wachezaji wamesha chanja ni asilimia 2 tu ndio mpaka sasa hawajachanja, pia kuna sintofahamu ya Champions League, Europa League na Europa Conference League, World Cup play-off kama itachezwa nchini humo kutokana na tamko hilo la serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live