Wed, 12 Apr 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Afisa Habari wa Simba SC, amesema itakuwa ni aibu kubwa Yanga SC kutangazia ubingwa kwenye mechi yao ya Dabi itakayopigwa Jumapili, Aprili 16, 2023 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.
Ahmed amesema kwamba, klabu yao ina miiko yake hivyo hawatakubali kamwe kuona Yanga anashinda mbele yao.
"Itakuwa ni aibu kubwa, itakuwa ni fedheha kubwa. Itakuwa ni historia mbaya itakayodumu kwa vizazi na vizazi hivyo sisi kama Simba hatupo tayari kuona hilo linatokea," alisema Ahmed.
Ahmed ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuinadi mechi yao hiyo ambayo wao ni wenyeji.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live