Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ishu ya wachezaji Coastal Union bado ni moto

Coastal Union FCC Wachezaji wa Coastal Union

Thu, 1 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Baadhi ya wachezaji wa Coastal Union akiwamo mshambuliaji wake Maabad Maulid huenda wakajiweka kwenye wakati mgumu kutokana na kitendo cha kumpiga mwamuzi kwa chupa ya maji wakati wa mchezo na Azam FC.

Katika mchezo huo uliopigwa Novemba 27 kwenye Uwanja wa Azam Complex wachezaji wa Coastal Union hawakuridhishwa na mwamuzi Gilbert Mrina kutoka Kilimanjaro kuchezesha kwa dakika 102.

Mrina alichezesha dakika hizo baada ya dakika 90 kumalizika na kuongezwa nne ambazo hazikuchezwa kutokana na kipa wa Coastal Union, Mahamoud Mroivili kutumia kulalamika kwamba aliumia.

Akizungumza na Mwanaspoti jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi nchini, Nassoro Hamduni alisema suala la nyongeza au kufidia dakika zilizopotea liko chini ya mwamuzi.

“Ushauri wangu kwa wadau wa soka ni kusubiri vyombo vya mpira (Bodi na Kamati) vitakaa na kuangalia tukio na endapo kutakuwa na uvunjifu wa sheria wahusika watachukuliwa hatua.”

“Kuna vyombo vinavyosimamia ambavyo vitaangalia na kutoa taarifa rasmi kwenye lile jambo, sisi kama kamati tutapata taarifa kutoka kwenye vyombo ambavyo vimeundwa rasmi kwa ajili ya jambo hilo.”

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPLB) ambaye ni Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mnguto alisema tukio lililotokea litafikishwa kwenye Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kwa ajili ya kujadiliwa.

“Mimi ndiye Mwenyekiti wa Kamati hii lakini linapokuja suala linaloihusu Coastal Union huwa siruhusiwi kuhusika kwenye kikao hivyo tusubiri maamuzi yatakayochukuliwa,” alisema.

Juzi, Maabad aliliambia Mwanaspoti kuwa kilichotokea siku hiyo kilitokana na mwili kupata joto kutokana na ugumu wa mechi hiyo na kujikuta kuingia kwenye changamoto hiyo.

Chanzo: Mwanaspoti