Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ishu ya vibali kocha wa Simba mambo bado

Coach Hitimana Kocha msaidizi wa Simba, Thierry Hitimana

Sun, 3 Oct 2021 Chanzo: salehejembe.blogspot.com

Kocha Msaidizi wa Simba Hitimana Thiery, raia wa Rwanda mambo bado hayajakuwa sawa kuhusu ishu ya vibali vya kazi.

Hitimana alitangazwa kuwa Kocha Msaidizi wa Simba bado hajakaa kwenye benchi la ufundi la timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Dider Gomes kutokana na kukosa vibali vya kazi.

Taarifa zimeeleza kuwa suala hilo kwa sasa linashughulikiwa na muda wowote itajulikana hatma yake ya kupata vibali vya kutendea kazi.

"Mwalimu Hitimana suala lake la vibali vya kazi bado halijapatiwa ufumbuzi kwa sababu viongozi walikuwa wanasubiri timu iweze kurudi Dar ilipokuwa Dodoma kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji na tayari timu imesharudi hivyo itafahamika hivi karibuni," imeeleza taarifa hiyo.

Kwa upande wa Hitimana kuhusu ishu hiyo alisema kuwa hawezi kuzungumzia jambo lolote kwa kuwa kuwa suala hilo linashughulikiwa na uongozi.

Chanzo: salehejembe.blogspot.com