Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ishu ya jezi feki, Simba na Yanga msikimbilie polisi - Waziri Kijaji

Mwehhh Ally Kamwe.

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Viwanda, Uwekezaji na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji amewataka Wafanyabiashara kuacha kukimbilia Polisi pale wanapopata changamoto ya kibiashara badala yake waende Tume ya Ushindani (FCC).

Dkt. Ashatu ameyasema hayo jana baada ya kutembelea na kukagua ghala lililobainika kuhifadhi jezi bandia za timu za Azam FC, Yanga SC, Simba FC na timu ya Taifa Tanzania.

Waziri huyo amesema Taasisi ya kwanza inayotakiwa kupelekewa malalamiko ni FCC kwa sababu ndiyo yenye mamlaka ya kulinda watumiaji kubaini bidhaa ni bandia au sio bandia, lakini pia kulinda ushindani wenye ufanisi katika biashara.

Aidha, Dkt. Ashatu ametoa siku saba kwa Mkurugenzi wa tume hiyo Wiliam Erio kujiridhisha na kujua idadi halisi ya T-shirt na jezi zote zilipo ili kuhitimisha jambo hili na kushughulika na watu wasioitakia mema Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: