Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ishu ya Mutale na jezi ya CAF

Joshua Mutaleeee Ishu ya Mutale na jezi ya CAF

Thu, 19 Sep 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ishu ya winga wa Simba, Joshua Mutale kuvaa jezi namba 26 katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF), timu hiyo ikicheza dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya, ilikuwa ni kuchelewa kubadalisha katika mfumo.

Jezi namba saba anayoivaa Mutale katika Ligi Kuu Bara, katika michuano ya CAF ilikuwa inatumiwa na aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Willy Essomba Onana ndiye jina lake lilipelekwa CAF kabla ya kumtema.

Mutale alifafanua ishu hiyo; “Jina la Onana ndilo lilikuwa limepelekwa CAF kuvaa jezi namba saba, ndio maana ikawa ngumu kuitumia namba hiyo, badala yake nikavaa jezi namba 26.”

“Katika mechi za Ligi Kuu nitaendelea kuivaa jezi hiyo namba saba, ila kimataifa nitakuwa navaa 26 hadi itakapobadilishwa katika mfumo Januari kupitia usajili wa dirisha dogo iwapo tukiingia makundi,” aliongeza.

Mutale alisema jambo kubwa kwake ni kujituma, ili mchango uwe muhimu katika timu, hivyo suala la jezi kwa sasa sio ishu ya kumfanya asicheze vizuri.

“Jambo la msingi ni kufanya majukumu ninayoambiwa na kocha, kuhusiana na jezi kuvaa 26 badala ya saba kimataifa ni suala la muda kila kitu kitakaa sawa,” alisema Mutale.

Katika mchezo huo Simba ilitoka suluhu, jambo ambalo Mutale alisema wanaamini watapambana marudiano, ili kupata ushindi Jumapili.

Chanzo: Mwanaspoti