Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ishu ya Magoma na Yanga imefungwa hivi

Sakata La Mzee Magoma Zc Ishu ya Magoma na Yanga imefungwa hivi

Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said, Kamati ya Utendaji ya Yanga na Bodi ya Wadhamini wanaendelea na majukumu yao yote kama kawaida kwa sababu waliingia madarakani kupitia katiba halali iiyopewa baraka na Serikali pamoja na TFF ›› (FCC, BMT).

Young Afticans Sports Club imefungua kesi ya jinai katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Juma Magoma na wote waliohusika kughushi saini za wajumbe wa Bodi ya wadhamini, Mama Fatma Karume na mzee Jabil Katundu.

Pia, Magoma na wenzake watapelekwa mbele ya mkutano Mkuu kama ni wanawachama halali mkutano mkuu utachukua hatua ya kuwafuta uanachama kwa mujibu wa katiba ambayo inakataza masuala ya kikatiba na Migogoro yoyote ya kimpira ndani ya Yanga kupelekwa mahakamani.

Yanga SC imeiaandikia barua Mahakama isongeze mbele muda wa Klabu hiyo kufanya mapitio ya kesi kwa sababu haikuwahi kushiriki kwenye kesi hiyo.

Kwa nini mahakama ilitoa hukumu bila uwepo wa washitakiwa mahakamani? Kwa kuwa maombi ya mleta maombi (Juma Magoma) hayakupingwa, Mahakama ilikubaliana na nafuu zote zilizoombwa kwenye hati ya madai (plaint).

Maana yake washitakiwa Yanga SC hawakushiriki katika kesi hiyo tangu ilipofunguliwa Nov 2022 kabla ya Hersi Said na uongozi uliopo kuingia madarakani.

Msingi wa kesi Mnamo 6/11/2022, Juma Magoma na Geofrey Mwipopo walifungua kesi dhidi ya Wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa Yanga kwa madai kuwa hawalitambui baraza la wadhamini la Klabu hiyo wakidai liliingia kwa mujibu wa Katiba ya 2010 ambayo wanadai haijasajiliwa.

Agosti 2, 2023 Mahakama ya Kisutu ilitoa hukumu ikiwa imesikiliza upande mmoja, hukumu hiyo haikutekelezwa na Yanga.

Mei 2024 Magoma na wenzie walipeleka maombi ya kukazia hukumu kwa Hakimu Mkazi Kisutu, kuomba Mahakama kulifuta baraza la wadhamini wa Yanga na kuutoa uongozi wa Yanga na kutaka wakabidhiwe timu na Asset zote za Yanga waendeshe wao.

Wao wanaamini katiba ya mwaka 1968. Katiba iliyofanyiwa marekebisho 2011 na 2021 hawaitambui kwa hiyo mambo yote yaliyofanyika kuanzia 2010 hadi leo waaliiambia mahakama iyabatilishe. Kwa maana hiyo, viongozi wote hadi makombe yote tangu 2010 ni batili.

Mahakama ikithibitisha kuwa kuna kesi ya Jinai ya kughushi saini, Mzee Magoma na wenzake watakumbana na adhabu kali kwa mujibu wa sheria za nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live