Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ishu ya Benzema na Nuno Espirito ipo hivi

Nuno X Benzema Ishu ya Benzema na Nuno Espirito ipo hivi

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Inadaiwa Karim Benzema na kocha wake Nuno Espirito Santo walizinguana kwenye chumba cha kubadilishia nguo kabla ya kocha huyo kufukuzwa kazi.

Katika taaarifa ya kushtua iliyotolewa na Jarida la Al Riyadiah, kulitokea ugomvi mzito kati ya Benzema na Nuno Espirito ambapo imechangia kwa kiasi kikubwa kufukwa kwake kazi Al-Ittihad.

Ripoti hiyo inaeleza mvutano ulizingira nafasi ya Espirito Santo umekuwa ukitokota, baada ya Benzema kudaiwa kuwasilisha mapendekezo kwa bodi kuwa meneja huyo anakwamisha maendeleo ya klabu hiyo.

Nuno Espirito alifutwa kazi Al-Ittihad, licha ya kuwapa ubingwa wa Saudia msimu uliopita, kikosi chake kinashika nafasi ya sita kwenye Saudi Pro League msimu huu, licha ya kuwa na mastaa wa maana kikosini, akiwamo straika Karim Benzema na kiungo N’Golo Kante.

Al-Ittihad ilichapwa 2-0 na Al-Quwa Al-Jawiya ya Iraqi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Asia jambo lililowavuruga mabosi wa timu hiyo, ambayo pia ipo nyuma ya vinara wa ligi ya ndani Al-Hilal kwa pointi 11 baada ya mechi 12. Kipigo kutoka kwa Al-Quwa Al-Jawiya kimeripotiwa kumfanya kocha huyo atibuane na wachezaji wake kwenye vyumba vya kubadilishia, akiwamo Benzema.

Na ripoti zinafichua kwamba huenda mabosi hao wakamfungia kazi kocha mwenye maneno mengi, Jose Mourinho ili akafanye kazi kwenye mikikimikiki ya Saudi Pro League. Kocha mwingine anayetajwa kuwa kwenye mipango ni Julen Lopetegui.

Klabu hiyo pia inadaiwa kuvutiwa na kocha wa zamani wa Ufaransa Laurent Blanc huku ikimfikikira kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane.Nuno, 49, alichukuliwa na Tottenham mwaka 2021 baada ya miaka minne ya kuinoa Wolves.

Huko Spurs alidumu kwa miezi minne tu, akafukuzwa baada ya kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Manchester United, ambapo kilikuwa kipigo cha tano kwa Spurs katika mechi saba.

Al-Ittihad ilifanya maboresho makubwa kwenye kikosi chake katika dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi baada ya kutumia zaidi ya Pauni 100 milioni kuwanasa mastaa kama Benzema, Kante, Fabinho, Luiz Felipe na Jota (sio yule wa Liverpool).

Chanzo: Mwanaspoti