Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ishu ya Awesu kwenda Yanga ipo hivi

Awesu Yangaaaa Ishu ya Awesu kwenda Yanga ipo hivi

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa KMC FC, umesema milango yao ipo wazi kwa timu yoyote inayohitaji kumsajili kiungo wao, Awesu Awesu kwa msimu ujao.

Kauli hiyo ni baada ya kuwepo wa tetesi za kiungo huyo kuingia kwenye rada za Yanga kwa wachezaji wazawa kwenda kuongeza nguvu kwenye safu ya viungo.

Mtendaji Mkuu wa KMC, Danie Mwakasungula amesema bado Awesu ni mchezaji halali wa KMC na thamani ya mchezaji huyo wataweka wazi timu inayohitaji kumsajili kiungo huyo.

Amesema milango ipo wazi kwa klabu au timu yoyote inayohitaji kumsajili Awesu au mchezaji yoyote yule ambaye amevutiwa naye wapo tayari kufanya biashara.

“Mpira wa miguu ni biashara, Yanga au timu nyingine wanahitaji huduma ya Awesu au mchezaji yoyote hapa kwetu tupo tayari kukaa meza moja kwa lengo la kufanya biashara hiyo kwa kuangalia maslahi kwa pande zote,” amesema Mwakasungula.

Ameomgeza kuwa ofa ya Awesu itakuwa ni baina ya pande zote tatu kwa kuangalia maslahi ya mchezaji na klabu kwa sababu ni mchezaji muhimu na tegemeo kwa kikosi cha timu hiyo.

Mwakasungula amesema tayari wamepokea ripoti na kuanza kufanyia kazi mapendekezo ya wachezaji wapya kwa ajili ya maboresho ya kikosi cha msimu ujao.

Ameweka wazi nafasi wanazoangalia ni kuimarisha safu ya ulinzi na kuimarisha safu ya ushambuliaji kuleta watu wenye ubora wa kusaidia timu hiyo msimu ujao kufanya vizuri na kutoa changamoto kwa klabu kubwa nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live