Baada ya meneja wa Arsenal, Mike Arteta kumwaga cheche dhidi ya mwamuzi Andy Madley na VAR, mkuu wa waamuzi, mkongwe wa zamani, Howard Webb ametangaza kukutana na mameneja wote wa timu zinazoshiriki Ligi kuu ya England.
Madley pamoja na waamuzi wa VAR wana tuhumiwa na Arteta kwa kuwanyima penalti mbili katika mchezo huo ambao timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
Matokeo hayo hayakumfurahisha Arteta, wachezaji, viongozi na mashabiki wa klabu hiyo kwani yameinyima ushindi na pia kuipunguzia pointi mbili dhidi ya timu ya Manchester City ambayo inashika nafasi ya pili.
Mpaka sasa, Arsenal FC ina pointi 44 zilizotokana na mechi 17 wakati Manchester City ina pointi 39. Newcastle United ipo katika nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi 35 sawa na klabu ya Manchester United huku Tottenham Hotspurs ikimalizia orodha ya timu tano bora kwa kuwa na pointi 33.
Webb ambaye ni boss wa Chama cha Waamuzi cha England (PGMOL) alisema kuwa maamuzi hayo yamemfadhaisha na kuna ajenda za siri dhidi ya timu yake yenye lengo la kutwaa ubingwa msimu huu. Alisema kuwa haingii akilini kuona waamuzi wanashindwa kutafsiri sheria pamoja na kupewa jukumu kubwa la kuchezesha mechi hiyo muhimu, kwani ilikuwa inahusisha timu zilizopo kwenye tano bora.
“Najivunia wachezaji wangu, walicheza vizuri na kutawala mchezo pamoja na mchezo kuwa na matukio mengi ambayo yangeweza kutupatia ushindi, lakini penalti mbili zilikuwa za wazi na tulistahili kupata,” alisema Arteta.
“Tulipolalamikia kuhusu maamuzi hayo, mwamuzi alikuwa mkali kwetu, mimi nazungumzia kilichotokea katika mechi na wala siyo kitu kingine,” alisema.
KILICHOTOKEA
Katika dakika ya 59, kiungo mshambuliaji wa timu ya Arsenal, Bukayo Saka alipiga pigo la adhabu ndogo kutoka wingi ya kulia na kuchezwa na mchezaji wa Newcastle, Nick Pope.
Hata hivyo, Gabriel Magalhaes alifanyiwa faulo na Dan Burn ndani ya eneo la penalti. Pia mchezaji wa Newcastle, Jacob Murphy alishika mpira, na mwamuzi na ‘watu wa VAR’ walifunika tukio hilo dhidi ya Arsenal.
SHERIA INASEMAJE?
Tukio la kwanza:
Kwa mujibu wa sheria namba 12 ya soka, Burn alivuta jezi ya Gabriel na ikuwa penalti. Hivyo mwamuzi wa VAR, Stuart Attwel hakuweza kuamua hivyo pamoja na ukweli kuwa kati ya penalti 15 kwenye EPL zilizopitia VAR, saba zilikuwa za kushika mpira, saba zilikuwa za faulo mbalimbali na moja ilitokana na mchezaji kuvutwa jezi.
Wiki iliyopita beki wa AFC Bournemouth Adam Smith alimvuta jezi mshambuliaji wa Chelsea Christian Pulisic na VAR haikufanyia marejeo tukio hilo pamoja na rekodi kuonyesha kuwa mwamuzi wa VAR, Lee Mason ndiye pekee aliyewahi kuamuru pigo la penalti katika tukio kama hilo.
Tukio la pili
Ni wazi kuwa Murphy alishika mpira ndani ya eneo la penalti kisheria ilikuwa penalti. Hata hivyo kama nilivyosema katika matoleo yaliyopita, mwamuzi anaweza kuwa na mtazamo wake au tafsri kuhusiana na tukio hilo kwa kuzingatia kuwa mkono wa Murphy ulikuwa eneo asilia au hapana.
Yapo matukio kama hayo ambayo maamuzi yake yalikuwa penalti na bado yalizua utata mkubwa na kuna mengine ambayo maamuzi yalikuwa tofauti na penalti na utata na hoja mbalimbali zilikuwepo.
MAPENDEKEZO YA WEBB KWENYE VAR
Webb amependekeza maamuzi karibu yote ya uwanjani yafanywe na waamuzi wanaosimamia mechi husika na VAR itumike tu pale ambapo inaonekana kuna tatizo ambalo linahitaji maamuzi ya kina ili kuondoa utata. Webb amesema kuwa wahusika wa VAR wanatakiwa pia kumuuliza mwamuzi wa mechi kuhusiana na tukio husika na kupata mtazamo wake kisheria pamoja na kuangalia picha za marejeo.
“Kwa mfano, kwa tukio la Gabriel na Burn, mwamuzi alitakiwa kuuliza kama mchezaji anayedaiwa kufanyiwa faulo ilikuwa sahihi au si sahahi kuliko kuamua moja kwa moja kuwa si halali na kuendelea na mchezo,” alisema.
Alisema kuwa pamoja na VAR kuwa na malalamiko mengi tofauti, bado kuna maeneo ambayo teknolojia hiyo imepatia pamoja na ukweli kuwa maamuzi mengi ya mechi yanaaanzia kwa mwamuzi kuwa sahihi. “Kelele nyingi ninazo sikia zipo kwenye EPL. Ni wazi kuwa kuna ‘tuta’ katika njia hii ambalo linatakiwa kutafutiwa utatuzi.”