Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Irankunda mbongo anayefananishwa na Sadio Mane

Irankundaaaaa Irankunda mbongo anayefananishwa na Sadio Mane

Tue, 26 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kasi, nguvu na maarifa ndio mambo matatu ambayo yamemfanya Nestory Irankunda ambaye alizaliwa Kigoma, Tanzania kabla ya kuhamia Australia pamoja na familia yake kama wakimbizi, kufananishwa na nyota wa kimataifa wa Senegal, Sadio Mane aliyepita kwenye klabu ambayo imemsajili wiki chache zilizopita ya Bayern Munich.

Huu ni wakati wake, Nestory mwenye miaka 17 anazungumzwa mno na vyombo vya habari vya Australia na hata Ulaya tangu Novemba 14 mwaka huu ambapo iliripotiwa kufanywa makubaliano ya kuuzwa kwa Bayern Munich kwa uhamisho pauni 3 milioni (zaidi ya Sh 9.5 bilioni) pamoja na nyongeza wenye uwezekano wa kuvunja rekodi ya uhamisho wa ligi hiyo, iliyowekwa na Marco Tilio wakati akijiunga na Celtic.

Hii ni safari ya kusisimua, kutoka Tanzania, Australia hadi Munich ambako atatua Julai mosi mwakani kwa ajili ya kuanza maisha yake mapya ya soka kwa mabingwa hao wa kihistoria Ujerumani.

Jochen Sauer, mkurugenzi wa maendeleo ya vijana wa Bayern, anasema, “Tumekuwa na uhitaji wa Nestory kwa kipindi kirefu na tumefurahi tumefikia makubaliano naye pamoja na klabu yake ya Adelaide United juu ya kuhamia Munich kwa msimu ujao wa joto.”

Hakuishia hapo anaendelea kumuongelea kwa kusema, “Tunatoa shukrani nyingi na za dhati kwa klabu yake kutokana na mazungumzo mzuri ambayo yalifanyika, Nestory ni winga mwepesi sana, mpiga chenga hodari na mmaliziaji mzuri. Tumeshawishika na uwezo wake ni wakati kwake wa kupiga hatua zaidi.”

Irankunda mwenye nafasi ya kuichezea timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kutokana na kuzaliwa kwake hapa licha ya wazazi wake kutokea Burundi, kwa sasa anaichezea timu ya taifa la Australia chini ya miaka 17 lakini hilo halimfungi kubadili uamuzi wake kwa kuichagua kuichezea Taifa Stars au Burundi ambako wanatokea wazazi wake.

Winga huyo amichezea Adelaide United zaidi ya mechi 39 katika kikosi cha kwanza hadi sasa, akiwa amefunga mabao tisa na kutoa pasi nne za mabao, na anatarajia kuongeza idadi hiyo hadi mwisho wa msimu huu.

NI MANE MTUPU

Nestory Irankunda atakwenda Munich msimu ujao atakapofikisha umri wa miaka 18. Wale ambao wamemwona akicheza na timu ya taifa la Australia kwa vijana wenye chini ya umri wa miaka 17 au kwenye ligi wanamfananisha na Sadio Mane, mchawi wa Senegal ambaye alionyesha makali yake kwenye Ligi ya England akiwa na jezi ya Liverpool.

“Mchezaji ambaye siku zote nimekuwa nikimlinganisha naye ni Sadio Mane. Ana urefu sawa, kasi sawa, nguvu sawa, na wote wana uwezo mzuri wa kupiga mashuti. Wote pia wanapenda kushambulia kwa kuwafuata mabeki,” anasema skauti, Sacha Pisani aliyehojiwa na tovuti ya transfermarkt.

Anaendelea kumuongelea, “Tangu mwanzo wake, Nestory Irankunda amekuwa kama mashine ya kushangaza. Tangu alipofunga bao ambalo nililiona kama la kichawi kwa njia ya frii-kiki ya moja kwa moja akiwa na umri wa miaka 15, Nestory amekuwa na nguvu kasi kiasi cha kushangaza sana. Adelaide, imekuwa sehemu nzuri kwa ukuaji wake chini ya usimamizi wa kocha Carl Veart, ni kama amefunikwa kwa pamba kwenye masikio yake ili asilewe sifa za mashabiki ambao wamekuwa wakimsifu kila uchao.”

MAISHA BINAFSI

Irankunda alisoma Parafield Gardens huko Parafield Gardens, Australia Kusini, katika kitongoji cha kaskazini mwa Adelaide. Licha ya kudaiwa kutofanya vizuri shuleni, Irankunda alisema somo lake alilopenda zaidi lilikuwa Kiingereza.

Kinda huyo alikuwa shabiki wa kutupwa wa Barcelona ya Hispania na alikuwa akivutiwa kwa ukaribu na Carles Puyol na Gerard Pique ambao walimfanya kupenda kucheza nafasi ya beki wa kati utotoni kabla ya kubadilishwa.

Chanzo: Mwanaspoti