Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Iran yampokonya paspoti nyota wa soka

FE62BAC7 97E9 4D53 B6C4 126DBA24C55C.jpeg Iran yampokonya paspoti nyota wa soka

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Iran imempokonya hati ya kusafiria nyota wa zamani wa soka Ali Daei, vyombo vya habari vya hapa vimeripoti jana Jumatatu, baada ya kukosoa ukandamizaji wa waandamanaji wanaopinga mauaji ya Mahsa Amini.

Iran imekumbwa na maandamano ya nchi nzima tangu kutangazwa kifo cha mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 22, Septemba 16, siku tatu baada ya kukamatwa jijini Tehran kwa tuhuma za kukiuka sheria za mavazi za nchi.

Septemba 27, Daei aliitaka serikali ya Iran "kutatua matatizo ya wasnanchi wa Iran badala ya kutumia ukandamizaji, nguvu na ukamataji".

"Kuchukuliwa kwa paspoti ya Ali Daei kunatokana na alichoandika Instagram kuhusu kifo cha Mahsa Amini," gazeti la mageuzi la Hammihan limeripoti.

Akiwa na jina la utani la "Shahriar" (Mfalme wa Farsi), mshambuliaji huyo wa zamani alishikilia rekodi ya kufunga mabao mengi katika mechi za kimataifa, akiwa na mabao 109, hadi September 2021, wakati Cristiano Ronaldo alipompiku.

Daei, 52, alikuwa mmoja wa wachezaji wa kwanza wa Iran kucheza kwenye ligi ya Ulaya, akiwa amechezea kwanza Arminia Bielefeld kabla ya kujiungana Bayern Munich na baadaye Hertha Berlin.

Chanzo: Mwanaspoti