Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inzaghi atoa neno kujiunga Man United

Simioni Inzaghiiii Kocha mkuu wa kikosi cha Inter Milan Simion Inzaghi

Sat, 9 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa kikosi cha Inter Milan Simion Inzaghi baada ya kuhusishwa kujiunga na kikosi cha Manchester United ameweka wazi kuwa kwasasa mipango yake ni kukinoa kikosi chake cha Inter Milan.

Inzaghi kwasasa anaongoza Ligi na kikosi chake cha Inter Milan kwa takribani alama 11 mbele ya timu inayomfuata katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi kuu nchini Italia "Serie A".

"Najihisi vizuri hapa, klabu hii, vijana hawa, na mashabiki wake."

"Hakuna sababu ya kuongelea hilo, bado tuna tuna miaka mitatu ya kuweka akili yetu kwenye ushindi, hatujali chochote, klabu yoyote inatutaka tuendelee kucheza kama hivi."

Vyombo vya habari nchini Italia vinaripoti kuwa kocha huyo licha ya kuhitajika na Manchester United, Liverpool na Barcelona zote kwa pamoja zinamhitaji.

Inaelezwa kuwa Inzaghi anafuraha ya kuendelea kusalia Inter Milan na anatarajiwa kuongeza mkataba hadi 2027.

Manchester United huenda ikaachana na kocha wake Erik Ten Hag msimu wa joto .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live