Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inter yamalizana rasmi na Eriksen

Chrstian Eriksen Inter Mailand 2021 1627018374 67726 Christian Eriksen

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Inter Milan imethibitisha kuachana na aliyekuwa mchezaji wa klabu hiyo, Christian Eriksen. Haya ni maridhiano baina ya pande zinazohusika.

Eriksen amekuwa nje ya uwanja kwa muda toka alipopata matatizo ya moyo akiwa kwenye majukumu ya Timu ya Taifa kwenye mashindano ya Euro 2020. Kufuatia tatizo hilo, Eriksen amewekewa mashine kwenye mfumo wake wa moyo.

Kwa mujibu wa Serie A, ligi hiyo hairuhusu mchezaji mwenye matatizo kama hayo kucheza kwenye ligi hiyo na hivyo, Inter pamoja na Eriksen, wamefikia makubaliano ya kukatisha mkataba kati yao.

Kufuatia kusitisha mkataba wa Eriksen, mchezaji huyo sasa yupo huru kuamua klabu nyingine atakayoitumikia nje ya Serie A ambapo kwa kanuni za Serie A haruhusiwi kucheza ligi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live