Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inter yakwea kileleni Serie A

Inter Milan 65dbc77 Inter yakwea kileleni Serie A

Sat, 7 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Italia Serie A Inter Milan wamelazimika kutokea nyuma kwa bao mbili na kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Empoli katika mchezo uliochezwa Ijumaa.

Ushindi wa Inter Milan ambayo ipo kwenye ushindani wa ubingwa na wapinzani wa karibu AC Milan unawafanya kukwea mpaka nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi.

Empoli ilianza kufunga bao kupitia kwa Andrea Pinamonti, kabla ya Kristjan Asllani kuweka kambani bao la pili ingawa Simone Romagnoli alishindwa kuondosha vyema mpira na kujiweka kambani kabla ya mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Lautaro Martinez kuweka kambani mara mbili.

Jioni kabisa mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Barcelona na Manchester United Alexis Sanchez aliingia kambani na kufunga bao la nne na kufanya matokeo kuwa 4-2 baada ya dakika 90.

Kwa matokeo hayo, Inter wanaenda kileleni kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya AC Milan ingawa wamecheza mechi moja zaidi, AC Milan watacheza Jumapili dhidi ya Verona wanaweza kurudi kileleni endapo watashinda mechi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live