Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inter na Ac Milan Kujenga Uwanja Mpya “Cathedral”

Serie A Italian Match Thumb Cbssports 05 Ac Milan V Inter Milan AC Milan na Inter Milan

Wed, 22 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vilabu vya Inter na Ac Milan wameungana katika mradi mpya wa kutaka kujenga uwanja mpya ambao wamepanga kuupa jina la “Cathedral” ambao umechorwa na mchoraji ambaye aliyebuni uwanja mpya wa Tottenham Hotspur Stadium.

Uwanja mpya utajengwa wilaya moja ambao upo uwanja wa San Siro jijini Milan, mpaka sasa bado hawajaweka wazi uwezo wa uwanja huo ila inatarajiwa kuwa mashabiki watakuwa karibu sana na kiwanja tofatauti na San Siro.

Ujenzi huo utahusisha zaidi ya square metres 110,000 ikijumuisha eneo la kuchezea maduka na miundombinu mingine ambayo inaweza kuwa ni sehemu za wazi au watashirikiana na jiji la Milan kujua nini kinaweza kufaa kwa ajiri ya matumizi.

Kwa sasa klabu zote, Inter na Ac Milan wameshakubaliana na ubunifu wa uwanja huo na mamlaka za jiji limethibitisha mradi huo jukumu limebaki kwa vilabu hivyo kuweza kumaliza maswala ya ndani, huku ikitarajiwa kuwa mwaka 2022 watamaliza kila kitu na kutangaza rasmi kila kiti kuhusu uwanja huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live