Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inter Milan yatinga Robo Fainali UEFA

Inter Vs Porto Inter Milan yatinga Robo Fainali UEFA

Wed, 15 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya kupata ushindi mwembamba kwenye mechi ya raundi ya kwanza, Inter Milan imefanikiwa kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kulazimisha sare tasa na FC Porto kwenye mechi ya raundi ya pili iliyochezwa Jumanne.

Matokeo ya sare tasa yalikuwa na faida kwa Inter ambao walishinda bao 1-0 katika mchezo uliochezwa wiki moja iliyopita dimba la San Siro ambapo sasa inakuwa mara ya kwanza kwa Inter kufuzu nane bora tangia mwaka 2011.

Isivyokuwa bahati kwa FC Porto wakiwa kwenye mapambano ya vita mmoja ya wanajeshi wake alisalimu amri kwa kuonyeshwa kadi nyekundu, huyo ni winga wa Kibrazil Pepe.

Inter Milan inaungana na Manchester City kwenda robo fainali ambapo zitasubiri wapinzani wake kwenye droo ya Ijumaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live