Rais wa lnter Milan, Javier Zanetti amekiri kwamba amependezwa na mwanzo mzuri wa timu hiyo msimu huu baada ya kushinda mechi tatu mfululizo.
Inter iliweka rekodi kali ya kutoruhusu bao huku ikishinda mechi mfululizo tangu msimu ulipoanza mwezi uliopita.
Tuna furaha sana kuona timu ikifanya vizuri, tunashukuru kuna baadhi ya wachezaji wameondoka, ambao walifanya mambo makubwa hapa, lakini wamekuja wachezaji wapya na wamejitoa kwa ajili ya timu, tumeshinda mechi tatu mfululizo, tuna uwezo wa kushindana kwa ajili ya ubingwa wa Serie A msimu huu.” Bosi huyo alisema
Wakati huohuo Mshambuliaji wa zamani wa Inter, Antonio Cassano alisisitiza msimu huu watabeba ubingwa wa Serie mzuri tangu msimu ulipoanza.
Kauli hiyo imekuja kufuatia rekodi iliyowekwa hivi karibuni kabla ya mapumziko kupisha mechi za kimataifa.
Cassano alisema: “Ushindi wa mechi tatu mfululizo? sishangai, Inter inacheza mpira mzuri sana.
Ndio maana napata hasira, tulivyopoteza ubingwa wa Serie A mara mbili mfululizo, miaka miwili iliyopita Inter ilikuwa hatari sana. Lakini mwaka huu tuna malengo ya kubeba ubingwa.”
Pia, Cassano alidai kwamba alizungumza na Kocha wa Inter, Simone Inzaghi kuhusu mambo mbalimbali ya klabu: “Kocha kaiweka timu katika mazingira mazuri ina uwezo wa kufanya makubwa, lakini tusisifu sana kwa sababu msimu uliopita hatukuambulia kitu.”