Kwenye Intelijensia ya soka sasa mambo yamebadilika, Tegemea mambo kadhaa, Kwanza baada ya draw kufanyika, klabu yenye idara nzuri ya Intelijensia inaanza kutafuta reaction.
Watu wa taifa husika wamewapokeaje, tena kama huku Tanzania hizo reaction tunazipeleka kwenye pages zao hukohuko, mfano post ya juzi ya Mamelodi vs Yanga ndio post yenye engagement kubwa zaidi kwenye Instagram yao, kwa nini?
Kwa sababu wameigusa timu yenye wafuasi wa kutosha wanaotumia mitandao na Wapinzani wao pia, so pale mpinzani anajua namna walivyopokelewa.
Mbali na haya ndio wakati ambao idara ya intelijensia inakua Busy kufuatilia mechi za live zinazochezwa na mpinzani wao kwasasa na mikanda ya mechi ya nyuma, Wanatafuta ubora na uimara.
Hakuna details wataidharau. Ndio muda ambao Watatembelea sana kurasa za timu pinzani kusoma presha yao kwao, kama wataweza basi ni kutafuta mazoezi ya mwisho kuelekea mechi kwa kuweka Camera katika uwanja ambao mpinzani atapasha siku moja kabla ya mchezo.
Huu ndio muda Gamondi na Benchikha wanatakiwa kupokea ripoti ya kitengo hiki na benchi linachora ramani ya vita, Kazi ya benchi la ufundi inarahisishwa sana na kitengo cha intelijensia.
Timu kua na Mafanikio ni zaidi ya kikosi kizuri na mashabiki wengi.
Je, chama lako lina hili eneo, wanalifanya kwa ukubwa gani?