Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inspekta Hashimu kusimamia Simba, AS Vita

Usalama Pic Data Inspekta Hashimu kusimamia Simba, AS Vita

Thu, 25 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limemteua Inspekta Hashimu Abdallah kuwa Ofisa usalama wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Simba dhidi ya As Vita. Simba anatarajiwa kuwa mwenyeji wa As Vita Aprili 3 mwaka huu katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam. Katika mchezo huo Simba inatakiwa kupata matokeo au kutoka sare ili kujikatia tiketi rasm ya kutinga robo fainali katika michuano hiyo. Mpaka sasa Simba ina pointi 10 na imesalia michezo miwili pekee dhidi ya As Vita sambamba na Al Ahly ambapo Simba itamfuata Nchini Misri. Ikipata matokeo katika mchezo huo itakuwa na pointi 13 au ikitoka sare itakuwa na pointi 11 ambapo itakuwa na tiketi ya robo fainali. Simba iko kundi A hivyo katika michezo miwili iliyosalia itafikisha pointi 16 endapo itashinda huku Al Ahly akishinda pia michezo miwili atakuwa na pointi 13 wakati As Vita akishinda nae atakuwa na pointi 10 na Al Merrikh atakuwa na saba. Kutokana na uwiano huo Simba inabidi apambane kadri awezavyo kupata matokeo katika mchezo huo ili apate uhakika wa kutinga hatua hiyo.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz