Kiungo wa Juventus, Paul Pogba ameingia kwenye orodha ya mastaa wanaohitajika na matajiri wa Saudi Arabia katika dirisha hili.
Taarifa zinaeleza kwamba Al Ittihad ya Saudi Arabia imeweka mezani ofa inayofikia mshahara wa Euro 100 milioni kwa mwaka ili kuhakikisha inampata Pogba.
Hata hivyo, hadi sasa hakuna chanzo chochote kilicho karibu na Pogba kilichothibitisha suala hili na baadhi ya vyanzo vimedai hakuna ofa rasmi iliyowasilishwa kwa wawakilishi wa mchezaji huyu.
Ittihad ni miongoni mwa timu zilizosajili mastaa kadhaa wenye majina makubwa barani Ulaya ikiwa ni pamoja na N’Golo Kante na Karim Benzema.
Mambo yanazidi kupamba moto baada ya Pogba kuonekana Saudia, lakini hakuna uhakika wa asilimia mia ikiwa alikuwa huko kukamilisha dili au ishu zingine.