Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inonga aweka rekodi yake Bongo

Inonga Simba Yanga Inonga aweka rekodi yake Bongo

Wed, 19 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Henock Inonga, beki wa Simba ameweka rekodi yake ya kuwa beki wa kwanza kufunga ndani ya Kariakoo Dabi kwa msimu wa 2022/23.

Ndani ya dakika 180 watani hawa wa jadi walipokutana kwa msimu huu ni mabao manne yamefungwa huku Simba ikifunga mabao matatu na Yanga ikiwa imetupia bao moja.

Inonga ni beki pekee ambaye amefunga bao la mapema zaidi ikiwa ni dakika ya kwanza akitumia pasi ya beki mzawa Shomari Kapombe na bao la pili ni mali ya Kibu Denis ambaye ni kiungo.

Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa kwanza uliochezwa Oktoba 23 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 1-1 Simba.

Mabao yalifungwa na viungo ambapo kwa Simba ni bao la Augustine Okrah alipachika bao dakika ya 14 akitumia pasi ya Clatous Chama.

Kwa upande wa Yanga wao bao lao lilipachikwa dakika ya 45 na kiungo Aziz Ki ambaye alipiga pigo huru lililomshinda mlinda mlango wa Simba, Aishi Manula.

Rekodi nyingine ambayo beki huyo ameandika ni kuwa namba moja kwa watupiaji mabeki ndani ya ligi akiwa na mabao matatu akifuatiwa na Yannick Bangala na Bakari Mwamnyeto hawa wa Yanga wametupia mabao mawilimawili kila mmoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live